Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ridhiwani ashiriki Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amemwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Februari 11, 2025 Jijini Dodoma Katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre.

Aidha, Maadhimisho hayo yanalenga kuhamasisha Wanawake na Wasichana kujumuishwa katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati na kuhamasisha wafanya maamuzi kuwashirikisha wanawake katika masuala ya sayansi.

Mwaka huu 2025 Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo kufungua fursa za kazi za STEM: Sauti ya Mwanamke katika Taaluma na Kazi za Kisayansi.