Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Waziri Sangu ashiriki mazishi ya Marehemu Jenesta Mhagama


Waziri wa Nchi, IOfisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (Mb), ameshiriki katika ibada ya misa ya mazishi ya marehemu Jenista Mhagama iliyofanyika Jumanne, tarehe 16 Desemba 2025, katika Parokia ya Mtakatifu Andreas, kijiji cha Ruanda, wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma.

Mazishi hayo yaliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye aliwaongoza mamia ya waombolezaji kutoka mikoa mbalimbali katika tukio la kuhifadhi mwili wa marehemu.

Itakumbukwa Marehemu Jenista Mhagama amewahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.