Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ridhiwani akabidhi hundi ya Tsh. Milioni 730 kwa Vikundi vya Vijana, Vijana na Wenye Ulemavu


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amekabidhi hundi ya shilingi Milioni 730 kwa Vikundi 74 vya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu kutoka Halmashauri ya Muheza, jijini Tanga ambayo inatokana na mikopo ya asilimia 10 kupitia mapato ya ndani.

Akizungumza leo Februari 9, 2025 wakati wa kukabidhi hundi hiyo, amesema utaratibu wa kutoa Mkopo kwa makundi hayo umekamilika hivyo kwa sasa kikundi au mtu mmoja anayekidhi vigezo ataweza kunufaika na Mkopo huo.

Mhe. Ridhiwani amebainisha kuwa, vikundi vilivyonufaika na mkopo huo vimepatuwa elimu ya ujasiriamali na matumizi mazuri ya pesa ili kukua zaidi na kuepuka changamoto zilizokuwepo awali ikiwemo kubadilisha matumizi ya Mkopo huo na kufanyia mambo mengine hivyo kupelekea wakopaji kutorejesha pesa hizo kwa wakati au kushindwa kulipa kabisa.

Amesema Serikali ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwezesha makundi mbalimbali mikopo yenye riba nafuu ikiwemo mikopo ya asilimia 10.

Katika hatua nyingine, Mhe. Ridhiwani amewataka wanufaika wa mkopo huo kurejesha pesa hizo kwa wakati ili wengine waweze kukopeshwa.