News
Waziri Mkuu Majaliwa amwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino
WAZIRI MKUU, Mhe. Kassim Majaliwa leo Juni 13, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino yanayofanyika katika uwanja wa Mwanga Centre, mkoani Kigoma.
Katika Maadhimisho hayo Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete , Naibu katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mkuu wa mkoa huo, viongozi wa TAS na SHIVYAWATA.
Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo kimataifa ni ‘Kudai Haki Zetu, Kulinda Ngozi Zetu, Hifadhi Maisha Yetu’.
Aidha, Kitaifa, kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni: “Ushiriki katika Uchaguzi ni Haki Yetu: Kuchagua na Kuchaguliwa, Linda Haki za Watu Wenye Ualbino.”