Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WAZIRI MHAGAMA AONGOZA KIKAO CHA MASHAURIANO KWA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA WAMILIKI WA MAKAMPUNI SEKTA YA ULINZI BINAFSI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi na Wamiliki wa Makampuni ya Ulinzi Binafsi walipokutana kwenye kikao cha Mashauriano kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano PSSSF, Februari 12, 2021 Jijini Dodoma.

Sehemu ya viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi na Wamiliki wa Makampuni ya Ulinzi Binafsi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho cha mashauriano.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akieleza jambo wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.

Kaimu Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri, Bi. Pendo Berege akieleza jambo wakati wa kikao hicho cha Mashauriano kilichowakutanisha viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi na Wamiliki wa Makampuni ya Ulinzi Binafsi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA), Bw. Isaya Maiseli akichangia mada wakati wa kikao hicho cha Mashauriano kilichowakutanisha viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi na Wamiliki wa Makampuni ya Ulinzi Binafsi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi wakiimba wimbo wa Mshikamano “Solidarity” walipokutana kwenye kikao cha Mashauriano kuhusu sekta hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano PSSSF, Februari 12, 2021 Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi na Wamiliki wa Makampuni ya Ulinzi Binafsi walipokutana kwenye kikao cha Mashauriano kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano PSSSF, Februari 12, 2021 Jijini Dodoma. Kulia aliyekaa ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.