Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Kikwete: Serikali Kuendelea Kuchochea Maendeleo ya Vijana kwa Kuwawezeshan Ujuzi wa Kumudu Soko la Ajira


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuchochea maendeleo ya vijana kwa kuhakikisha vijana wanaohitimu katika ngazi mbalimbali za elimu nchini wanakuwa na ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuajiriwa ili waweze kujiletea maendeleo.

Amefafanu kuwa, Katika kuhakikisha vijana wanakuwa na ujuzi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeendelea kuwawezesha vijana mafunzo ya stadi mbalimbali kupitia Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi ambazo zitawasaidia kujiajiri na kuajiriwa na hatimaye kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa taifa.

Mhe. Kikwete amesema hayo leo Februari 26, 2025, wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Nambala Wilayani Mbozi mkoani Songwe mara baada ya kuzindua vyumba vya madarasa, wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani humo.

Mhe. Waziri Kikwete ameongeza kuwa Serikali imeboresha sekta ya elimu kali
kwa kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 imetenga shilingi trilioni 1.2 pamoja na kufanya maboresho ya sera ya elimu na mafunzo ambayo imejikita katika kutoa elimu ujuzi unaowezesha vijana kujitegemea.

Naye, Mkuu wa mkoa wa Songwe,Mhe.Daniel Chongolo amefafanua kuwa shughuli za sekta ya elimu katika mkoa huo zimeboreshwa kutokana na Rais Samia kutoa fedha za utekelezaji wa mahitaji ya mkoa huo,
ambapo mkoa huo umeweza kuimarisha mazingira na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wanafunzi wa shule ya sekondari Nambala na Ileje wasichana wameishukuru serikali kwa ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa jambo ambalo litawapunguzia msongamano mkubwa darasani.

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri Kikwete ametembelea Wilaya ya Ileje na Mbozi ambapo amezindua vyumba vya madarasa 11 katika shule ya sekondari ya wasichana Ileje, Jengo kisasa la halmashauri ya Ileje na Shule ya awali na msingi Forest.