Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wadau wapigwa Masasa kuhusu Mwongozo wa Taifa wa Utambuzi wa Mapema


Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Rasheed Maftah amefungua Kikao cha Mafunzo ya Kujengewa Uelewa Juu ya Mwongozo wa Taifa wa Utambuzi wa Mapema na Afua Stahiki kwa Watoto Wenye Ulemavu, tarehe 9 Juni, 2025 Morogoro.

Amesema kuandaliwa kwa mwongozo huo kutawezesha kupata huduma za Marekebisho mapema, kuelimisha jamii kuepuka mila na imani potofu zinazochangia ukiukwaji wa haki za Watoto wenye ulemavu na kuongeza uelewa katika jamii kuhusu umuhimu wa lishe kwa Mama Mjamzito ili kuepuka mtoto kuzaliwa na ulemavu.

Aidha, Mkurugenzi Maftah amesema matarajio yake baada ya mafunzo hayo ni kuona Watoto wenye ulemavu wanajumuishwa katika uandaaji wa Programu zitakazoandaliwa katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri kwa ajili ya kupata huduma stahiki kulingana na aina ya ulemavu walionao.

Pia, kuhuhisha taarifa za Watoto Wenye Ulemavu watakaotambuliwa na kupewa huduma katika mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Taarifa zanWatu wenye Ulemavu (PD-MIS).

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Maafisa lishe, Maafisa Elimu maalum, Maafisa ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa kutoka dawati la ulinzi na usalama, Viongozi wa dini, Taasisi/Mashiriki yanayohudumia watu wenye ulemavu na Afisa Afya.