News
Wadau sekta binafsi wapigwa msasa matumizi ya Mfumo wa soko la Ajira
Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, wamewajengea uwezo wataalamu wa taasisi za binafsi kuhusu mfumo wa Mfumo wa Taifa wa Taarifa za Soko la Ajira (NLMIS).
Akizungumza leo Februari 11, 2025 kwenye mafunzo hayo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Alana Nchimbi amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuratibu, kukusanya, kuchambua na kuweza kutangaza taarifa za soko la ajira kwa wakati.
Vile vile, amesema kupitia mfumo huo waajiri watapata fursa ya kutangaza nafasi za kazi sambamba na kuwasiliana na wahitaji wa ajira wenye sifa stahiki kwa njia rahisi kupitia mfumo huo.
Wakitoa maoni kwa nyakati tofauti wadau walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru serikali kwa mfumo huo na kueleza kuwa wataweza kuingiza data na kuzifikia kwa wakati taarifa za soko la ajira ambazo zinamtazamo wa kitaifa.
Pia, wametoa wito kwa waajiri nchini kutoa ushiriano kwa serikali ili kuendelea kukuza mahitaji ya soko la ajira nchini.