Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wachimbaji Wadogo wa Madini 200 Wanufaika na Mafunzo ya Ukuzaji Ujuzi


Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yawapiga msasa wachimbaji wadogo wa Madini 200 Mkoani Geita ili kuongeza ujuzi wa shughuli wanazofanya.

Aidha, Mafunzo hayo yanatolewa ni utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi hiyo ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya Madini nchini kwa kuhakikisha wachimbaji hao wanafanya kazi kwa weledi na ujuzi stahili.

Akifungua mafunzo hayo, leo Juni 23, 2025 Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi hiyo Daudi Silasi, amesema mafunzo hayo yanalenga kuboresha usalama kazini, kuongeza ufanisi na tija, kuhifadhi mazingira, kuongeza mapato na maendeleo ya kiuchumi, kufanikisha urasimishaji ujuzi pamoja na kuwajengea uwezo wa kibiashara.

Mafunzo hayo ya wiki moja na yanahusisha wadau wa mbalimbali wa Sekta ya Madini ikiwemo Wizara ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Buckreef Gold Company Limited na TGC.