News
Vyombo Vyama vya Wafanyakazi waaswa kuboresha ustawi wa Vyama vyao
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus amesema Mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya wafanyakazi yana faida kubwa kwa kuzingatia majukumu yenu hasa kwa upande wa Usimamizi na Maamuzi mnayolazimika kuyafanya kwa kufuata Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya wafanyakazi Leo tarehe 17 Februari, 2025 Mkoani Morogoro.
Serikali chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kushughulikia masuala ya Watumishi na wafanyakazi kwa ujumla.
Aidha, waajiri kufuata na kuzingatia Miongozo yote ya Ajira ya Kitaifa na kimataifa ikiwemo kuwapa uhuru wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi pasipo kuwaingilia katika maamuzi yao.
Vile vile, amewataka viongozi hawo kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Miongozo ya kazi iliyopo ili kuepuka migogoro ambayo inaweza kuchangia kushuka kwa uzalishaji sehemu za kazi.
Awali, Msajili wa vyama vya wafanyakazi Donald Alacka kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amesema Mafunzo hayo yanalenga kuwakumbusha viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia Sheria na Taratibu zilizopo.