Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Tanzania na Qatar kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Kazi na Ajira


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kazi wa Qatar Dkt. Ali Bin Saeed Bin Samikh kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya sekta ya kazi na ajira ili kuwezesha Watanzania kunufaika na fursa za ajira nchini Qatar .

Viongozi hao wamekutana leo Januari 29, 2025 Riyadh nchini Saudi Arabia ambapo wameelekeza timu ya Wataalam inayohusisha pande zote kukutana haraka kutathmini utekelezaji wa hati ya makubaliano kati ya Tanzania na Qatar iliyosainiwa mwaka 2014 nchini Qatar.