Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

NAIBU WAZIRI KATAMBI ATEMBELEA MIRADI YA VIJANA WALIOWEZESHWA MIKOPO YA ASILIMIA 4 KUPITIA HALMASHAURI


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akiangalia mageti ambayo yanatengenezwa na Kikundi cha Vijana cha Mshikamano kinachojishughulisha na Uchomeleaji na utengenezaji wa bidhaa za Chuma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kufuatilia utekelezaji wa mkopo wa asilimia 4 inayotolewa kwa vijana kupitia halmashauri zilizopo nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akiangalia mkataba wa kikundi cha Vijana cha Mshikamano kilichokopeshwa Milioni 40 na Halmashauri ya Kahama. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho Bw. Harry Ramadhan.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Uchumi Viwanda, Bw. Mogeni Kubalunga (kushoto) akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kushoto) alipotembelea kikundi hicho ikiwa ni sehemu ya kufuatilia utekelezaji wa uwezeshaji wa mkopo wa asilimia 4 inayotolewa kwa vijana kupitia halmashauri zilizopo nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akiangalia urembo wa gypsum alipotembela kikundi cha Vijana cha Uchumi Viwanda kilichopo eneo la Majengo, Halmashauri ya Kahama ili kujionea shughuli za uzalishajimali za vijana.

Muonekano wa mikanda ya gypsum inayotengenezwa na kikundi cha vijana cha Uchumi Viwanda kilichopo eneo la Majengo, Halmashauri ya Kahama.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana cha Jipapanue kinachojishughulisha na shughuli za Ufugaji na kilimo alipotembelea kikundi hicho ikiwa ni sehemu ya kufuatilia utekelezaji wa uwezeshaji wa mkopo wa asilimia 4 inayotolewa kwa vijana kupitia halmashauri zilizopo nchini.