Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Naibu Waziri Ikupa Aipongeza JAMAFEST Kushirikisha Wenye Ulemavu


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshugulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa amelipongeza Tamasha la Utamaduni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) kwa kuwazingatiaa watu wote wenye mahitaji Maalumu kwa kuwapa kipaumbele katika Tamasha hilo.


Ameseyasema hayo leo, mbele ya Waandishi wa Habari, mara ya baada ya kutembelea Mabanda na kujionea ubufunifu mbalimbali ya maonyesho ya Tamasha la JAMAFEST, linaloendelea kufanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Amewapongeza Waandaji wa Tamasha la JAMAFEST kwa kuwapa kipaumbele watu wenye Ulemavu katika kuwapatia mabanda, kwa ajili ya kuuza na kuonyesha bidhaa zao katika Tamasha hilo na kuweza kutangaza biashara zao

“Nitoe Pongezi kwa Waandaji wa Tamasha hili la JAMAFEST, Muitikio wa watu umekuwa mkubwa hasa kwa kundi la watu wenye ulemavu, nimejionea vitu vingi vinavyotengenezwa na walemavu, bidhaa zao ni nzuri kabisa na zipo kwa viwango vya juu sana” Alisema Mhe. Stella Ikupa


Sambamba na hilo Mhe Ikupa Amewataka Watanzania kufika katika Viwanja vya Taifa kujionea bidhaa mbalimbali za kiutamaduni zinazo tengezwa na Watanzania ili waweze kujua Utamaduni wa Watanzania na Wanaafrika Masharikikwa ujumla.

Pia Mhe. Ikupa amewasisistiza Watanzania kutumia muda wao mwingi kujionea mambo mbalimbali ya Utamaduni yanayo fanyika katika Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST


“Ukifika kwenye Tamasha hili la JAMAFEST hautajuta kupoteza huo muda wako, ila utakuwa umepata kitu kikubwa cha kujifunza juu ya Utamaduni wa Muafrika” Alisema Mhe. Stella Ikupa

Aidha katika Ziara hiyo Mhe. Ikupa amewakabidhi baiskeli za watu wenye mahitaji maalum ndugu Martini Vicente mkazi wa Kigamboni na Ndugu Rajabu Ismail mkazi wa Magomeni- Mwembe Chai ambao wote ni Walemavu wa Miguu.