Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Sangu asisitiza ushirikiano kwendana na kasi ya Rais Samia


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kwa watumishi wa Ofisi hiyo ili kwenda na kasi ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi kwa wakati na kwa ufanisi.

Akizungumza katika hafla ya mapokezi iliyofanyika leo Novemba 17, 2025 Mtumba Jijini Dodoma amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mkazo kwenye uwajibikaji na utoaji wa huduma bora, hivyo watumishi wanapaswa kuongeza bidii na kufanya kazi kwa kushirikiana ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.

Mhe. Sangu amesema ushirikiano na mawasiliano mazuri katika maeneo ya kazi ni nguzo muhimu ya kuongeza ufanisi, huku akihimiza watumishi kuendelea kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu ya kila siku.

Aidha, amewahakikishia watumishi kuwa Ofisi yake itaendelea kuimarisha mazingira ya kazi, Ajira na Mahusiano ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakwenda sambamba na dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuleta mageuzi Chanya na maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Rahma Riadh Kisuo, amewapongeza watumishi wa Ofisi kwa mapokezi mazuri na kuwaahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu.

Katika hafla hiyo Mhe. Waziri Deus Sangu ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka pamoja na Katibu Mkuu, Mary Maganga.