Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Ridhiwani Kikwete : Ushirikiano wa Watumishi ni nguzo ya Mafanikio


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amewahimiza watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kushirikiana ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa katika kuhudumia wananchi.

Akizungumza leo, Februari 6, 2025, katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma, Mhe. Ridhiwani amesema ushirikiano umechangia ofisi hiyo kupata mafanikio makubwa katika kuleta ustawi wa sekta ya kazi, maendeleo ya vijana, masuala ya ajira na huduma kwa Watu wenye Ulemavu chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, amempongeza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mary Maganga, kwa uongozi thabiti unaoleta hamasa kwa watumishi na kutekeleza majukumu yao kwa bidii na weledi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Mary Maganga amewataka watumishi kuzingatia nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi.