Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Ridhiwani Kikwete ashiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu Soko la ajira


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Soko la ajira tarehe 29 Januari, 2025 Jijini Riyadh nchini Saudi Arabia.

Akizungumzia wakati akichangia hoja iliyowasilishwa kuhusu maendeleo ya vijana na mabadiliko ya kazi, Mhe. Kikwete alishukuru Ushirikiano uliopo baina ya wadau wa maendeleo ya kazi bila kusahau miongozo na mabadiliko ambayo yamefanyika nchini Tanzania ikiwemo mikakati ya kukuza ujuzi, matumizi ya TEHAMA, mkazo katika miradi inayotoa ajira nyingi na ile ya kimkakati.

Mkutano huo unawakutanisha Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka nchi zaidi ya 45 duniani kujadili na kuweka mikakati ya kuongeza kazi za staha kwa Vijana kwa kuzingatia mchango wa sayansi na teknolojia.