Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Maftah afungua kikao kazi kuhusu rasimu ya Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu


Mkurugenzi wa Kitengo cha watu Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Rasheed Maftah amefungua kikao kazi cha kupokea maoni kuhusu rasimu ya Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2025 kutoka kwa viongozi wa vyama, Taasisi pamoja na wadau wanao hudumia watu Wenye Ulemavu.

Ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam akimwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa kikao kazi cha kupokea maoni kuhusu rasimu ya Sera ya Taifa ya Watu Wenye ya Mwaka 2025.

Aidha, Amewapongeza viongozi wa vyama vya watu Wenye Ulemavu pamoja na Shirikisho la watu Wenye Ulemavu kwa kusimamia vyema masuala ya watu Wenye Ulemavu pamoja na kuona umuhimu wa kushiriki kikao hicho cha kutoa maoni ya rasimu hiyo.