Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AWATAKA WANANCHI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI


KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019, Mzee Ali amewataka wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wilayani Muheza mkoani Tanga kuhakikisha wanavitunza ili viweze kuwa endelevu.


Alitoa kauli hiyo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua mradi wa shughuli za uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ikiwemo kukagua mabanda ya wadau wa mazingira na kupanda miti eneo maalumu lillotengwa Kijiji cha Shembekeza.

Akiwa kwenye eneo hilo kiongozi huyo alionyeshwa kuridhishwa na namna mradi wa uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uharibifu wa vyanzo vya maji.


Alisema kwani Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji hivyo ni muhimu kulindwa na kuendelezwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Kiongozi huyo alisema suala la upatikanaji wa maji limekubwa na changamoto nyingi ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za serikali huku baadhi ya waka ndarasi wamekuwa wakichukua muda mrefu kukamilika miradi hiyo na hata wengine kukamilisha chini ya kiwango.

“Lakini pia niwaambie kwamba sio jambo jema kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji ikiwemo ukulima, ufugaji na kujenga karibu na vyanzo hivyo tushirikiane kuhakikiha tunatunza vyanzo vya maji ili vielendee kumudu kwqa vizazi vya sasa na vijazo”Alisema Kiongozi huyo.


Awali amkizungumza wakati akisoma taarifa ya miradi itakayozinduliwa na mwenge ikiwemo kukaguliwa Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema kwamba miradi yenye thamani ya Bilioni 29.471.7 huku akieleza kwamba mwenge huo umekimbizwa kwenye miradi na shughuli mbalimbali.

Alisema wakati wa mkesha wa mwenge huo huduma mbalimbali zilitolewa ikiwemo upimaji vvu ambapo walipimwa watu 448 ambapo kati yao wanaume 307 na wanawake 141 na waliokutwa na maambukizi ni wanaume wawili na wanawake wawili

Wakati huo huo Mpiga picha wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Muka Sabuni amepongeza na viongozi wa mbio hizo kutokana na namna aliyoweza kutengeneza mabango yenye picha zao wakati ulipoongia wilayani Muheza.


Hatua ya mmoja ya wakimbiza Mwenge ni kushangazwa na ubinfu uliotumiwa na mpiga picha huyo kwa kuweka picha zao kwenye mabango yaliyokuwa yamebeba ujumbe wa mwenge wilayani humo.

Kutokana na hali hiyo mmoja wa wakimbiza Mwenge hao Kenon alitumia muda wa makabidhiano baina ya Muheza na Pangani ndipo aliposimama na kumtambulisha huku akionyeshwa kufurahishwa na utendaji wake na kuiwataka viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kumtumia kwenye shughuli mbalimbali.