Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya bunge yapongeza kuanzishwa PSSSF Kiganjani


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq amepongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuanzisha Mfumo wa PSSSF kiganjani kwa lengo la kuwawezesha wanachama kupata taarifa za michango mahali popote walipo.

Mhe. Toufiq amebainisha hayo leo Februari 12, 2024 Jijini Dodoma baada PSSSF kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu namna ya kujisajili na kuanza kuitumia bila kutumia gharama za kusafiri kwenda ofisini kupata huduma.

Aidha, ametoa wito kwa Mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali juu ya kutumia Mfumo huo.

Awali akizungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amewapongeza wajumbe wa Kamati hiyo kwa kutenga muda kupata elimu na uelewa juu ya Mfumo wa PSSSF Kiganjani.