Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Zuhura Yunus ashiriki maadhimisho Miaka 30 ya TUGHE


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus ameshiriki katika maadhimisho ya miaka 30 ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) tangu kuanzishwa chama hicho.

Akizungumza wakati akimwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama hicho amesema serikali imepokea na itafanyia kazi hoja zilizotolewa ikiwamo kuendelea kuimarisha ukaguzi wa maeneo ya kazi kwa sekta binafsi.

“Mmependekeza Wizara iongeze bajeti na kuongeza idadi ya wafanyakazi katika idara ya kazi kwa lengo la kuboresha kaguzi katika maeneo ya kazi. Hili nimelipokea na litazingatiwa wakati wa maandalizi ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2025/26,” amesema

Awali, akisoma risala ya chama hicho, Katibu Mkuu wa TUGHE, Bw. Hery Mkunda ameomba ufanyike ukaguzi mahsusi kwa sekta binafsi kutokana na ajira nyingi ni za mikataba jambo ambalo linasababisha wafanyakazi kunyanyasika kwa kukosa uhakika wa ajira zao.

Vile vile, amesema ukaguzi huo utasaidia kubaini ukubwa wa tatizo na kufanya marejeo ya Sheria ili kuboresha eneo la aina ya mikataba ya ajira na adhabu kwa waajiri wanaozuia wafanyakazi kujiunga na vyama vyao.