Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wakulima wa Zabibu wanufaika na mafunzo ya Ukuzaji Ujuzi


Wakulima na wadau wa zao la zabibu wamenufaika na mafunzo ya Ukuzaji Ujuzi ambayo yamelenga kuwawezesha mbinu bora za kilimo na usindikaji wa zabibu.

Aidha, mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa wakulima hao leo Oktoba 22, 2025.

Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Godwin Mpelumbe amesema mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija na ubora wa mazao kupitia matumizi ya teknolojia na tafiti za kisasa katika sekta ya kilimo pamoja na kuzalisha kwa ufanisi na kuongeza thamani ya zao la zabibu nchini.

"Mafunzo haya ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi (Upskilling training) yatachochea ubunifu na kuimarisha uchumi wa wakulima wadogo na kuongeza mchango wa sekta ya kilimo katika kukuza pato la Taifa," amesema

Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu mafunzo hayo kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ambapo Wakulima wanapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo kutoka kwa wataalamu wa TARI kuhusu matumizi ya mbegu bora, utunzaji wa mashamba, na mbinu endelevu za kuongeza thamani ya zabibu kupitia usindikaji.