News
Waziri Ridhiwani ashiriki mjadala awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Desemba 5, 2024 ameshiriki katika Mjadiliano ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na wadau wa maendeleo kuhusu mustakabali wa Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).
Aidha, Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaandaliwa baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Mpango wa Kwanza na wa Pili ambapo kumekuwa na shuhuda mbalimbali kutoka kwa wanufaika ambao vipato vyao vimeongezeka kutoka hatua moja kwenda nyengine kwa kuoonesha shughuli walizo fanikiwa kuzifanya.