News
Waziri Ridhiwani afanya kikao na WCF
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amefanya Kikao na Wataalamu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Dkt. John Mduma katika Ofisi za Mfuko huo zilizopo jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadili kuhusu mapendekezo ya kuboresha malipo ya fidia kwa wafanyakazi, miongozo ya tathmini za ulemavu wa kudumu, utambuzi wa magonjwa yatokanayo na kazi pamoja na utoaji wa huduma za tiba na utengamao.
Mhe. Kikwete amehidi kuwa Wizara yake itaharakisha kutimiza takwa la kisheria la kutangaza mapendekezo ya kuboresha malipo ya fidia kwa wafanyakazi katika Gazeti la Serikali ili wafanyakazi wanaoumia au kupata magonjwa yanayotokana na kazi waweze kunufaika.