Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Waziri Ndalichako aridhishwa na kasi ujenzi chuo cha wenye Ulemavu Songea


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Chuo cha Wenye Ulemavu Songea na ametoa atoa pongezi kwa uongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa chuo hicho kwa ubora wa kazi inayoendelea kufanyika.

Mhe .Prof. Ndalichako ametoa pongezi hizoleo tarehe 28 Novemba, 2023 alipokuwa akikagua ujenzi wa chuo hicho ambacho kikamilikq madarasa, karakana, mabweni, Kituo cha maelezi ya Awali changamshi kwa watoto wadogo, Huduma za marekebisho, mabweni, maeneo ya michezo, bwalo, kumbi na jengo la utawala.

Aidha Prof. Ndalichako amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amedhamiria kuleta ustawi kwa watanzania na kutoa vipaumbele kwenye masuala ya Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara, Maji na kuwapa Afua stahiki zinazosaidia kundi la wenyeUlemavu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameishukuru serikali kwa ujenzi wa chuo hicho mkoani kwake kwani kitasaidia kuchochea maendeleo ya kielimu mkoani humo.