Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako aridhishwa maandalizi uzinduzi Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameridhishwa na maandalizi ya uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 utakaofanyika katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 2 Aprili 2024.

Ameyasema hayo leo tarehe 16 Machi, 2024 alipotembelea na kukagua ukarabati wa uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi pamoja na mafunzo wanayopatiwa vijana wa halaiki mkoani hapo kwaajili ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio hizo Mkoani hapo.

Mhe Ndalichako ameongeza kuwa Mkoa wa Kilimanjaro unanafasi kubwa ya kufanya vizuri kwakuwa maadhimisho hayo yanatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mbio za mwenge wa uhuru.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu".

Pia, amepongeza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwa na ushirikiano mzuri wakati wa maandalizi hayo.

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo ambaye ni Afisa Mipango Stephen Kivulenge amesema kuwa wamejipanga kwa uzinduzi huo.