Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wakuu wa Vyuo Wasisitizwa Upatikanaji wa Vitenda Kazi


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Said Mabie amewataka Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Stadi vilivyopitishwa na Serikali kutoa mafunzo ya Uanagenzi kuhakikisha vitendea kazi na malighafi za kufundishia zinapatikana kwa wakati ili vijana wajifunze kwa vitendo.

Aidha, amesema uwepo wa vitendea kazi unarahisisha uelewa, pia kuleta mchango mkubwa katika kuboresha kiwango cha ujuzi katika soko la Ajira na kuwezesha azma ya serikali ya kuwa na vijana wenye kuajirika ama kujiajiri wenyewe.

Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Said Mabie amesema hayo leo Desemba 28, 2023 Jijini Dodoma katika kikao cha kusaini hati za makubaliano za kutoa mafunzo ya uanagenzi awamu ya sita kwa wanafunzi 6000 wanaotarajiwa kuanza mafunzo Januari 2023.

Kwa upande mwingine, amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha za kuwezesha mafunzo hayo ambayo yanalenga nguvu kazi ya taifa hususan vijana kupata ujuzi ili waweze kufanya kazi kwa weledi.

“Tutapita kufuatilia utekelezaji wa mafunzo husika pamoja na viongozi wetu na mfahamu kwamba utekelezaji wa mafunzo haya utakuwa sambamba na ufuatiliaji wa mara kwa mara na kwa kina,” amesema.