Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Vijana wahimizwa kujiwekea akiba kwa manufaa ya sasa na baadae


VIJANA nchini wamehimizwa kutumia vizuri vipato wanavyopata kujiwekea akiba ili kumudu maisha yao ya sasa na baadaye.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Hifadhi ya Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Frank Kilimba, kwenye banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, katika Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya Huduma ya Fedha, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Novemba 21, 2023.

Bw. Kilimba amesema, Ofisi nya Waziri Mkuu inashughulika na makundi mabalimbali yakiwemo ya Vijana, Hifadhi ya Jamii na Wenye Ulemavu na kwamba wanayatumia maadhimisho hayo kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo kwenye Ofisi hiyo.

Alisema kupitia Halmashauri, Ofisi ya Waziri Mkuu inatoa mikopo kwa vikundi na mtu mmoja mmoja kulingana mradi uliobuniwa na kijana au kikundi husika.

Alisema mikopo inayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea vizuri ni nafuu sana kwa vijana kujikwamua katika biashara zao.

Wakizungumza baada ya kutembeela banda hilo, vijana kutoka wilaya za Longido, Ngorongoro na Simanjiro, wamesema elimu waliyoipata imewawezesha kujua fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu na kutoa ushauri kwa Halmashauri kutoa elimu zaidi ili kuwasaidia vijana kutambua fursa hizo.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa yameanza Novemba 20, 2023 na yatafikia kilele, Novemba 26, 2023, lengo hasa likiwa ni kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo Kiuchumi.”