Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Tanzania yaibuka mshindi wa tatu maonesho ya Juakali Jumuiya ya Afrika Mashariki


Mjasiriamali kutoka Tanzania ameibuka mshindi wa Tatu kwenye Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi au Jua kali yaliyomalizika jijini Juba, Sudan Kusini tarehe 5 Novemba 2024.

Mshindi wa Kwanza ametokea Kenya huku mshindi wa Pili akitokea Sudan Kusini.

Mjasiriamali huyo, Issa Mbogolume anayejishughulisha na uchoraji wa picha.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Bw. Issa Mbogolume amesema kuwa amefurahia ushindi huo ambao ni mkubwa kwake na kwa Tanzania na kwamba tuzo hiyo ni chachu kwake ya kuendelea kujituma zaidi na kuongeza ubunifu ili kulikamata soko la Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Aidha, Wajasiriamali 1,700 kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameweza kushiriki, ambapo kwa Tanzania wajasiriamali 299 wamegharamikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Sakia Suluhu Hassan, kushiriki maonesho hayo.

Maonesho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo, "Kukuza Ubunifu wa Kipekee na Maendeleo ya Ujuzi miongoni mwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki."