Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali yasema unyanyasaji dhidi ya Wenye Ulemavu sasa basi


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali haipendi kusikia na haitavumilia kusikia uwepo wa vitendo vya unyanyasaji kwa watu wenye ulemavu na wale watakaojihusisha na vitendo hivyo itawachukulia hatua kikamilifu.

“ Kitengo cha Ufuatiliaji na tathimini kiko ndani ya Ofisi hii ya Waziri Mkuu, kifanye ufuatiliaji kujua Ofisi na halmashauri zinavyotenga fedha kwa ajili ya makundi maalum na tupate taarifa ya ufuatiliaji wake,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Amesema haipendezi kuona tunakubaliana na kuweka maazimio ya kazi lakini utekelezaji wake unabaki katika makablasha.

Aidha, amewaelekeza Wakuu wa wote wa Mikoa nchini kutekeleza mpango kazi wa haki na ustawi kwa watu wenye ualbino na kuhakikisha unatekelezwa kikamilifu, kuhakikisha kila halmashauri nchini inatenga bajeti ya ununuzi wa Vifaa saidizi kwa kuzingatia uhitaji na viwango vya ubora wa Vifaa hivyo na Wizara za kisetka kutekeleza Mpango na mkakati huo kwa mujibu uliowekwa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI.