News
Serikali yaratibu Usaili wa Madereva 800 Ajira za Qatar kwa Ushirikiano na Mawakala Binafsi wa Ajira
Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira, imeratibu usaili wa madereva kwa kushirikiana na Mawakala wa huduma za ajira ikiwemo Mkapa foundation Imara Horizon, Connect General Supplies Co. Ltd, Sassy Solutions Co. Ltd na Larali Global Solutions kuhusu nafasi za udereva 800 zilizotangazwa kutoka nchini Qatar mwanzoni mwa mwezi Mei, 2025.
Aidha, Usaili huwo umefanywa na waataalum kitengo hicho, mawakala hao wa huduma za ajira, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji pamoja na wataalum kutoka nchini Qatar.
Katika uratibu wa zoezi hilo la usaili wa madereva lilikuwa na hatua tatu muhimu ambazo ni mahojiano ya ana kwa ana ambayo yamefanyika katika chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT), uendeshaji wa gari kwa vitendo katika maeneo mbalimbali ya barabara za Jiji la Dar es Salaam.