Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali kuendelea kushirikiana na TWCC, Trade Mark Afrika kuwezesha Vijana


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu imeahidi kuendelea kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) pamoja na Trade Mark Africa kupitia Tawi la vijana litakalo saidia kuwajengea uwezo wa kufikia malengo yao kupitia biashara.

Uzinduzi huo umefanyika Februari 13, 2024 Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpologo akimwakilisha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, wakati wa uzinduzi tawi hilo.

Aidha, Mpogolo ameipongeza TWCC na Trade Mark Africa kwa kuanzisha Tawi hilo linalolenga kuwasaidia vijana na wanawake kujengewa uwezo katika kukuza uchumi wa familia zao na Taifa kwa ujumla.