Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali itaendelea kuwalinda Wenye Ulemavu: Ridhiwani Kikwete


Serikali ya awamu sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwajali wenye ulemavu kupitia programu za uwezeshaji ikiwemo kuwapa mafunzo na kuwajumuisha katika fursa zinazotolewa na serikali.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa kufunga Mafunzo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa Watumishi wa Mahakama na Taasisi nyingine za Wenye Ulemavu leo Desemba 17, 2024 Jijini Dodoma.

Aidha, amesema Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uelewa wa masuala ya Usalama na Afya washiriki wenye ya changamoto ya ulemavu ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kuzingatia kanuni bora za kujilinda dhidi ya vihatarishi vya magonjwa na ajali mahali pa kazi.