Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali inatambua umuhimu wa Wanawake na Vijana katika kukuza uchumi wa nchi - Katambi


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatambua umuhimu na nafasi ya wanawake na vijana katika kukuza uchumi hususani katika sekta ya kilimo.

Mhe. Katambi amebainisha hayo Desemba 14, 2023 Jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa mpango wa AMDT wa ushauri kwa vijana na wanawake kwenye sekta ya kilimo biashara mwaka 2024 katika kubadilishana uzoefu wa mbinu za kuimarisha biashara baina ya wajasiriamali mahiri na wale wanaochipuki, lengo kuu likiwa ni kupiga hatua katika shughuli zao za kilimo biashara.

Amesema sekta ya kilimo inachangia asilimia kubwa katika pato la Taifa hivyo Wanawake na vijana ni chachu ya maendeleo kwenye Taifa lolote na hawapaswi kuwa nyuma au kusahaulika katika kukuza uchumi wa taifa hili bali wepewe mbinu na fursa za kuweza kufani kiwa kiuchumi.a

Aidha, ametoa rai kwa Taasisi za Maendeleo kuiga mfano wa AMDT katika kushirikiana na serikali kutatua changamoto mbalimbali za wajasiriamali wadogo ili waweze kujiinua kiuchumi.

“Niwashukuru washauri (mentors) kwa kuwekeza katika kuwainua wenzao, mmejipanga kuwa na wajasiriamali hawa chipukizi katika kipndi cha takribani miezi kumi kuwashika mkono, kuwatia moyo na kuwalekeza mbinu za kibiashara ili wapambane na kupiga hatua kutoka pale walipo” amesema.

Amesema Serikali ina nia ya dhati kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi na imeweka mikakati ya kuwajengea uwezo ili waweze kukabilia na changamoto zinazowakabili na waweze kujikwamua kiuchumi.