Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako azindua Mwongozo wa Mpango wa kushughulikia kero za Wastaafu


Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amezindua mwongozo wa Mpango wa kushughulikia kero za wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) nchini.

Mwongozo huo umezinduliwa leo tarehe 27 Novemba, 2023 mkoani Ruvuma katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,

Amesema kwa mwaka 2019 hadi 2023 serikali imelipa wastaafu jumla ya sh. Trilioni 2.17 ambapo makusudio ni kuhakikisha wanapata mafao yao kwa wakati.

"Kisheria wastaafu wanatakiwa kulipwa fedha ya kustaafu kutokana mshahara wake wa mwisho ambapo mwajiri anatakiwa kupeleka mchango mwezi mmoja baada ya mshahara wake"

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Wilman Ndile amesema kuzinduliwa kwa mpango huo kutasaidia kupunguza kero za wastaafu zinazofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii .

Naye Mkurugenzi wa Undeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mbaruku Magawa amesema kuwa mwongozo huo utawasaidia wanachama kutambua haki zao na kutatua changamoto zao kwa wakati.

Kwa niaba ya wastaafu Amen Ally ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali Wastaafu na kutatua kero zao.