Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako Ampongeza Rais Samia kwa Kuwezesha Vijana


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini vijana na kuwapa mitaji ya kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji mali.

Prof. Ndalichako amebainisha hayo Oktoba 10, 2023 katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa Mkoani Manyara ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama aliye mwakilisha Waziri Mkuu wa Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha, Prof. Ndalichako amesema Mhe. Rais ameanzisha mradi wa kilimo kwa vijana wa jenga kesho iliyo bora, kuanzisha mafuzo ya unenepeshaji mifugo na ufugaji wa samaki katika vizimba ili kupata ujuzi utakaowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Vilevile, Waziri Ndalichako amesema Mhe. Rais ametoa Shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya kuwezesha programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana ambapo mwezi Novemba vijana zaidi ya 4,500 watanufaika na mafunzo hayo.