Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako akipongeza Kiwanda cha Mbolea ITRACOM kwa Utekelezaji Sheria za Kazi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda cha mbolea cha ITRACOM Fertilizer Limited kwa kuzingatia sheria za kazi ikiwemo kuwapa mikataba wafanyakazi, Usalama na afya mahali pa kazi na kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wakati.

Prof.Ndalichako ameyasema hayo Septemba 18, 2023 alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Sheria za kazi, ambapo amewataka wawekaji nchini kuiga mfano kwa ITRACOM.

Waziri Ndalichako amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya wawekezaji nchini , uwekezaji wa kiwanda hicho cha mbolea umezalisha ajira za awali 1,198 na kitakapokamilika ajira moja za kwa moja 3500 zitazalishwa na ambazo sio za moja kwa moja zitazalishwa ajira 8000.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ameahidi kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili uwekezaji wa kiwanda hicho uweze kukamilika kwa wakati na kuwa na tija kwa wananchi.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kiwanda hicho, Kimaramuziro Nkurikiye ameshukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye ujenzi wa kiwanda hicho na kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo maji, Umeme, na Barabara.