Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako ahimiza weledi, ubunifu na ufanisi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Menejimenti ya Ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.

Prof. Ndalichako amebainisha hayo Desemba 12, 2023 Jijini Dodoma alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya (fungu 65) kwa kipindi cha Julaii hadi Novemba 2023.