Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ofisi ya Waziri Mkuu yatekeleza agizo la Mhe. Rais


Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan lililotolewa Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) Mkoani Morogoro la kumsaidia Bw. Leonard Msirikale Mwenye Ulemavu wa Uti wa Mgongo msaada wa kujikwamua kiuchumi. .

Akikabidhi Bajaji hiyo Desemba 14, 2023 Jijini Dodoma Msaidizi wa Rais masuala Maendeleo ya Jamii Ikulu Bi. Felister P. Mdemu amesema bajijai hiyo itamsaidia kujiingizia kipato na kujikwamua kiuchumi.

Aidha, ametoa rai kukitunza kifaa hicho na kuweka akiba ya pesa atazozipata kwa ajili ya kuendesha maisha yake ya kila siku ikiwemo kutunza familia, kusomesha Watoto Pamoja na majukumu mengine aliyo nayo.

Akizungumza katika Makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu Bw. Rasheed Maftah amempongeza Mhe, Rais kwa kuendelea kuwajali Watu Wenye Ulemavu kwa kuwapatia vitendea kazi na kuwawezesha kiuchumi.