Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ofisi ya Waziri Mkuu yaijengea uwezo Ethiopia utekelezaji Programu ya Kukuza Ujuzi


Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeujengea uwezo ujumbe kutoka Ethiopia kuhusu utekelezaji wa programu ya taifa ya ukuzaji ujuzi inayoratibiwa na ofisi hiyo.

Akizungumza Machi 12, 2024 Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi hiyo Pascal Vyagusa amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiratibu programu hiyo tangu mwaka 2016 kwa kutoa mafunzo kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa ikiwemo mafunzo ya uanagenzi, Urasimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo rasmi, mafunzo ya utarajali na kilimo cha kisasa.

Aidha, amesema ushirikiano wa nchi hizo utasaidia kuboresha maeneo ambayo ni kipaumbele katika uendeshaji wa programu hiyo na kuwezesha vijana kumudu ushindani wa soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Naye, Meneja wa Programu ya Ujuzi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Adame Traore amesema ILO itaendelea kuunga mkono serikali ya Tanzania kutekeleza programu hiyo.

Akizungumza Mshauri wa Wizara ya Kazi na Ujuzi kutoka Nchini Ethiopia Prof. Teshome Lemma amesema Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika Programu hiyo, hivyo uwezo waliojengewa utawasaidia kuendesha programu hiyo kwa weledi nchini kwao.