Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ofisi ya Waziri Mkuu na Kampuni ya Twiga wateta fursa za Ajira na uwezeshaji Vijana Migodini


TIMU ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wameanza ziara maalum ya kikazi katika migodi iliyopo chini ya Kampuni ya Twiga kwa ajili ya kuangalia namna inavyochochea uwezeshaji vijana, ajira na ukuzaji tija.

Akizungumza Novemba 27, 2023 katika Mgodi wa North Mara (Barrick), Mwenyekiti wa msafara wa Wakurugenzi hao ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukuzaji Tija wa Ofisi hiyo, Yohana Madadi, amesema lengo la ziara hiyo ni kufanya tathmini na kuangalia maeneo hayo na namna ya kushirikiana kuendelea kutengeneza ajira na kuwezesha jamii hususani vijana.

“Tumeona tija iliyopo katika uwekezaji huu kwa jamii, kwa serikali na kwa nchi kwa ujumla,"amesema.

Awali, Meneja Mahusiano wa Barrick North Mara, Francis Uhadi, ameeleza namna mgodi unavyotekeleza sera ya jamii (CSR) ikiwamo kuwezesha vijana kupitia fursa zilizopo kwenye mgodi na zinazozunguka kwenye maeneo yao.

Aidha, ujumbe huo umehusisha Mkurugenzi wa Huduma za Ajira, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Mkuu wa Mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ukuzaji Ajira na Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija.