Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mradi wa Rock City Mall kuchochea ukuaji uchumi Mwanza


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa uwekezaji mzuri na wenye tija mradi wa kitega uchumi wa jengo la biashara Rock City Mall uliopo jijini Mwanza.

Pongezi hizo zimetolewa na kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo leo tarehe 16 Machi, 2024.

Akizungumza, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq amesema uwepo wa mradi huo utasaidia kukuza thamani ya michango ya wanachama wa mfuko, kuongeza fursa za ajira na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

“Niipongeze Serikali kwa uwekezaji huu ambao ni njia moja wapo nzuri ya kuleta tija ya maendeleo na ustawi wa watanzania,” amesema

Aidha, Mhe. Toufiq amehimiza mfuko huo kuutangaza mradi huo ili wananchi waweze kutambua huduma zinazopatikana na kuongeza wigo wa wafanyabiasha katika jengo hilo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema serikali itaendelea kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii katika kuwekeza kwenye miradi yenye tija na ambayo itachagiza ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Abdul-Razaq Badru amesema kuwa mfuko huo umejipanga kuhakikisha fedha za wanachama zinakuwa salama na kukuza thamani kupitia uwekezaji wenye tija