News
Mhe. Ridhiwani aipongeza MM Connect kutoa fursa za Ajira kwa Vijana
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameipongeza kampuni ya MM Connect ambayo ni mdau wa kampuni ya simu ya Vodacom kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kutoa fursa za ajira kwa vijana wa nchini.
Aidha, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema fursa hizo za ajira kwa vijana zimesaidia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Amesema hayo wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa Wafanyakazi Bora wa MM Connect kwa mwaka 2024, jijini Dar es Salaam.
Kwa upande mwengine, Waziri Ridhiwani amewasisitiza wafanyakazi walipokea tuzo hizo kutumia fursa hiyo na kazi wanazofanya kukua kitaaluma lakini pia kufungua fursa ya kuchangia maendeleo ya nchi hususani eneo la TEHAMA.