Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi: Serikali imedhamiria kuboresha huduma kwa Watu Wenye Ulemavu


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa Serikali anayoiongoza Mhe. Rais Dkt. Samia imedhamiria kuendelea kuboresha huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ili kukuza ustawi wa kundi hilo.

Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau kuhusu majadiliano ya Programu ya Ujumuishwaji wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto mwenye Ulemavu uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Katambi amesema kuandaliwa kwa mtaala huo ni ishara ya kuunga mkono jitihada za serikali katika utekelezaji wa programu hiyo ambayo imejikita katika maeneo lishe, afya, ufunzaji wa awali, ulinzi na usalama pamoja na malezi yenye mwitiko.

"Dhamira ya serikali ni kuwekeza katika malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na kuhakikisha kuwa watoto wote nchini wanakua na kufikia utimilifu," amesema

Kwa upande mwengine, Mhe. Katambi amepongeza wadau kwa kuendelea kuunga mkono serikali katika kiwahudumia Watu wenye Ulemavu.