Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi: Rais Samia ameendelea kubuni Mikakati ya Kuwakwamua Vijana Kiuchumi


NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, amesema serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kubuni mikakati ya kuhakikisha vijana wanapata fursa za kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza Novemba 16, 2023 jijini Dar es salaam kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa vijana chipukizi iliyoandaliwa na Taasisi ya TEYA, Mhe.Katambi amesema fursa hizo ni pamoja na kuwapatia mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi kupitia programu ya Ukuzaji Ujuzi.

“Serikali inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira wezeshi ili kuwawezesha vijana walio katika sekta isiyo rasmi na wahitimu wa vyuo kuweza kujiajiri kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji mali hasa kilimo,”amesema.

Aidha, amesema ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata mitaji, Serikali imeboresha Mwongozo wa Utoaji Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) ambapo kwa sasa kijana mmoja mmoja anaweza kukopa.

“Niwashukuru waaandaaji wa tuzo niahidi serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote ambao wanatoa motisha kwa vijana na kuwahamasisha katika kuendeleza vipaji vyao,” amesema.