Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi Mifuko ya Pensheni kuhakiki Wastaafu kupitia Mifuko ya TEHAMA


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema Mifuko ya Pensheni nchini imeweka utaratibu wa kuhakiki wastaafu kwa kutumia mifumo ya TEHAMA.

Aidha, Mhe. Katambi amesema Mifumo ya uhakiki wa wastaafu kwa kutumia alama za vidole (Biometric Verification) imesaidia zoezi la uhakiki kwa wastaafu kufanyika kwa urahisi.

Ameyasema hayo bungeni Februari 14, 2024 alipokuwa akijibu swali la Mbunge, Mhe. Maimuna Pathan ambaye ametaka kufahamu kwa nini Serikali isifanye utaratibu wa kwenda kuhakiki wastaafu kwenye wilaya zao kuliko ilivyo sasa kuhakikiwa mikoani.

Kwa upande Mwengine, Mhe. Katambi amesema Serikali itaendelea kusimamia maboresho katika utoaji wa huduma kwa wastaafu ili kupunguza changamoto za kusafiri umbali mrefu na kuwapunguzia gharama zisizo na lazima.Mhe.