Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi ashiriki Mkutano wa sita wa Mwanamke Kiongozi


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Mwanamke Kiongozi uliofanyika leo Machi 6, 2024 jijini Dar es Salaam.

Aidha, zaidi ya wanawake 347 wameshiriki katika mkutano huo uliolenga kuwaleta pamoja Viongozi wa Taasisi Binafsi na Umma, Mashirika na Wadau kujadili masuala ya usawa wa kijinsia, Uongozi, Sera, Miongozo na Taratibu zinazochochea kuongeza idadi ya wanawake katika ngazi za uongozi sambamba na ushiriki wao katika nyanja za kiuchumi.

Mkutano huo umeongozwa na kauli mbiu isemayo "Wekeza kwa Wanawake: Ongeza kasi ya Maendeleo".

Vile vile, Mkutano huo uliambatana na Mahafali ya Awamu ya Tisa ya Programu ya Mwanamke Kiongozi (Female Future Programme).