News
Maafisa Ustawi wa Jamii, TEHAMA wapewa Mafunzo Mfumo PD - MIS
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetoa mafunzo ya siku 3 ya Mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji wa Taarifa na takwimu za Watu wenye Ulemavu (PD-MIS) kwa maafisa wa Ustawi wa jamii na maafisa Tehama wa Halmashauri (8) za jiji la Dodoma.
Akifungua Mafunzo hayo Januari 14, Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Maftah amesema utekelezaji wa mfumo huo ni miongoni mwa mafanikio makubwa nchini, kwa kuwa Tanzania imekua ya kwanza Afrika mashariki na kati kuanza kutumia mfumo huo.
“Utekelezaji wa mfumo huo ni maelekezo ya Mhe. Rais. Dkt Samia Suluhu Hassan aliyoelekeza tarehe 16 Machi, 2022 Ikulu Jijini Dodoma alipokutaka na Watu wenye Ulemavu,” amesema
Mafunzo hayo yanalengwa kutolewa kwa Maafisa Ustawi wa Jamii wote nchini, Maafisa Watendaji Kata na Vijijini ili waweze kusajiri Watu wenye Ulemavu katika maeneo yao.