Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Maadhimisho ya siku ya Wenye Ulemavu Kitaifa kufanyika Jijini Dodoma - Prof. Ndalichako


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Maadhimisho ya kilele cha siku ya watu wenye ulemavu kufanyika Desemba 2, 2023 jijini Dodoma.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Novemba 29, 2023 jijini Dar es salaam amesema madhimisho hayo yatakuwa daraja kati ya Serikali, Watu wenye Ulemavu, Wananchi na Wadau kutafakari kwa pamoja mafanikio, changamoto na fursa za kukuza ustawi wa Watu wenye Ulemavu.

Aidha amesema Maadhimisho haya yanatoa fursa ya kuhamasisha jamii katika nchi kutambua Haki, Fursa Usaawa, na Ushiriki wa Watu wenye Ulemavu katika Jamii, siasa na Uchumi.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote hususani wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika maadhimisho hayo.

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Wanawake na Watoto (SHIVYAWATA) Bi. Mzawa Jagame ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuthamini na kutambua umuhimu wa kundi hilo na kuendelea kutoa vipaumbele katika kila fursa zinapojitokeza.