News
Katibu Mkuu Maganga aongoza Kikao cha Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Programu ya SYP kwa Vijana Tanzania Bara na Visiwani
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mary Maganga tarehe 15 Mei, 2025 Jijini Dodoma ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za Kisekta Tanzania Bara na Visiwani zinazosimamia utekelezaji wa awamu ya pili ya program ya “Safeguard Young People” (SYP).
Ambapo lengo la kikao hicho ni kupokea utekelezaji wa programu ya Safeguard Young People (SYP) kwa 2024 na kuidhinisha utekelezaji wa mpango kazi wa programu hiyo awamu ya pili kwa 2025.
Aidha program hiyo inasimamiwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Uswiss Tanzania na UNFPA Tanzania.