Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kanzidata ya Vijana wa Halaiki mbio za Mwenge Kuanzishwa



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Eng. Cyprian Luhemeja amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itaanzisha kanzi data maalum itakayo tambua vijana wanaojitolea kushiriki halaiki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Eng. Luhemeja amesema hayo Oktoba 2, 2023 alipofanya ziara Mkoani Manyara kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mazoezi ya vijana hao ambapo ameridhishwa na mazoezi hayo.

Amesema kanzi data hiyo itasaidia kukuza vipaji vyao na kuandaa miradi itakayo wasaidia kuwakwamua kiuchumi ikiwa ni jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutambua nafasi ya vijana nchini.

Aidha ametoa wito kwa Makatibu Tawala nchini kuwaandaa vijana kuwa wazalendo kwa kuwafundisha historia ya nchi yao na kuwaanzishia programu za kuwainua kiuchumi hususani kwa wanafunzi wa msingi na sekondari wanaoshindwa kuendelea na masomo.

Sambamba na hayo, amewaahidi vijana wa halaiki wanao tarajia kushiriki katika kilele cha mbio hizo kutembelea Hifadhi ya Taifa Tarangire na kuwapatiwa vyeti vya pongezi ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao.